Alhamisi, 25 Aprili 2013

Jehanum ya Moto ni Wapi na Kukoje?


Miaka kadhaa iliyopita, nilikuwa nimezama sana katika dhambi. Nilipokuwa katika lindi hilo la dhambi, sikutaka kusikia chochote kwa mtu yeyote aliyenieleza kwamba niache dhambi, na eti niokoke. Niliwaona watu wanaohubiri mambo ya kuokoka, wameshindwa maisha, wamechanganyikiwa (frustrated), na tena

hawajasoma . Nakumbuka siku moja, mhubiri mmoja alinihubiri na kuniambia, ”Acha dhambi, au sivyo utatupwa katika Jehanum ya moto.“ Unajua nilimjibuje! Nilimwambia, ”Wewe usinibabaishe na hiyo Jehanum ya moto. Potelea mbali nikienda motoni, pilipili usizozila zakuwashia nini? Usinifuatefuate katika maisha yangu, chukua ”time“ yako!

Baada ya miaka kadhaa kupita, nilipokuja kusikia mafundisho kuhusu jinsi kulivyo huko Jehanum ya moto, nilikuja kufahamu kwamba yule mhubiri nilimjibu ”potelea mbali nikienda motoni“, kwa sababu tu sikuwa ninaelewa lolote kuhusu jinsi Jehanum kulivyo; kwa kuwa sikuwahi kufundishwa mafundisho hayo na kiongozi

wangu wa dini. Tangu niliposikia mafundisho hayo, maisha yangu yalibadilika kabisa. Mpendwa msomaji, huenda hata wewe hujasikia mafundisho halisi kuhusu jinsi kulivyo Jehanum ya moto, kama mimi nilivyokuwa; ndiyo maana nimeona leo nikushirikishe mafundisho haya kupitia katika tovuti hii. Mungu akubariki kwa kuendelea kusoma ujumbe huu.

Biblia inaeleza waziwazi kwamba mtu anapokufa, sekunde ileile ya kufa kwake anakabiliwa na hukumu. Tunasoma katika WAEBRANIA 9:27, ”Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu.“ Watu wanaofundisha kinyume na kweli ya Neno la Mungu, hufundisha kwamba mtu anapokufa, analala

tu, na hakuna lolote la hukumu mara moja wakitumia maandiko yafuatayo na kuyatafsiri visivyo: MATHAYO 27:52; 1WAKORINTHO 15:20: YOHANA 11:11-14 n.k.; na pia wanasema wafu hawajui lolote kwa kutumia maandiko kama MHUBIRI 9:5. Ilivyo ni kwamba, kinachobaki kaburini ni mwili tu. Roho ya mtu huondoka na kuingia katika mwili mwingine, unaoitwa mwili wa roho Miili tuliyo nayo wanadamu kabla ya kufa, inaitwa miili ya asili. Tunasoma katika 1WAKORINTHO 15:40, 44, ”Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani, …Ikiwa uko mwili wa asili, na wa r oho pia uko.“

Mwili wa asili, ndio unabaki kaburini, lakini roho ya mtu huondoka kama tunavyosoma katika MHUBIRI 12:7, Nayo mavumbi ya nchi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.“Mwili wa asili, ndio unaobaki kaburini, na huo ndio unaotajwa kwamba umelala, haujui lolote, na hauna kumbukumbu; lakini pasipo mwili huo, mtu atamwona Mungu na kukabiliana na hukumu yake dakika ileile baada

ya kufa (AYUBU 19:26). Ikiwa mtu ameishi katika mapenzi ya Mungu, mara tu baada ya kufa huchukuliwa mbinguni (LUKA 23:43; 16:22). Ikiwa ameishi na kufa katika dhambi, bila kutubu dhambi zake na kuokoka, hukumu yake mtu huyo, huwa ni kutupwa katika Jehanamu ya moto, mara tu baada ya kufa, kama yule tajiri anayetajwa katika Biblia (LUKA 16:19-24).

Mbinguni ni juu (Mbingu ya tatu), lakini kuzimu au Jehanamu ya moto, ni pande za chini zanchi (2 WAKORINTHO 12:1-4; MITHALI 15:1-4; MITHALI 15:24; ZABURI 63:9; EZEKIELI 31:14. Mara mtu anapokufa, hufika kwenye njia panda. Kila mmoja hupenda kwenda mbinguni kuzuri, hata hivyo ikiwa jina lake haliko katika kitabu

cha uzima cha mbinguni, hulazimika kwenda Jehanum ya moto. Mtu anayetakiwa kwenda motoni, huchachamaa na kukataa kwenda kwenye njia mbaya inayotisha ya motoni. Hali hii wakati mwingine inaweza kuonekana katika mwili wa asili kwa kumwangalia mtu anavyotapatapa na kuhangaika sana katika kufa kwake. Kutokana na mtu asivyopenda kwenda motoni na kutaka kwenda mbinguni asikotakiwa, mtu hulazimika kukamatwa kwa nguvu na malaika wa kutisha, na kutupwa katika Jehanum ya moto; inayojulikana pia kwa jina jingine, giza la nje; kama

tutakavyoona baadaye kidogo (UFUNUO 19:20; 20;10; MATHAYO 25:30).

Huko motoni Jehanum kukoje? Kunatisha, nashindwa hata nikueleze vipi unielewe. Moto wa milele, hatukuwekewa wanadamu bali shetani na malaika zake (MATHAYO 25:41). Kama utakwenda huko baada ya kusoma ujumbe huu, itakuwa ni kwa sababu ya kiburi chako tu, na kushupaza shingo yako na kukataa kulitendea kazi Neno hili (MITHALI 29:1). Moto wa Jehanum siyo mahali pa mchezo kama walimu wa uongo wanavyofundisha. Waalimu hawa huwafariji watu na kusema eti mtu ataunguzwa na moto na kutoweshwa na kuangamizwa kabisa na ndiyo mwisho wake. Wanatumia maandiko kama MATHAYO 10:28 (kuangamizwa) na YOHANA 3:16 (kupotea). Kuangamia katika maandiko hayo haimaanishi kumalizika kabisa, bali kukabiliwa na mauti (ESTA 4:16). Mauti ya watu walioko motoni, ni mauti ya milele, kama tutakavyoona hivi punde. Kondoo akipotea, haimaanishi hayupo kabisa ila ametengwa na mchungaji (ISAYA 57:1-3).

Vilevile, neno ”Kuharibu“ linapotumika kuhusiana na adhabu ya milele, halina maana ya kufanya kitu kisiwepo, bali ni kuadhibu vikali (1WAKORINTHO 3:16-17. Waalimu hawa wa uongo, pia hufundisha pia kwamba, eti watu watatoweshwa kama moshi baada ya kuunguzwa kwa kutumia andiko la ZABURI 37:20. Kutoweshwa hapa ni

kutenganishwa na Mungu, kama Adamu na Hawa walivyotoweshwa na kutolewa katika bustani ya Edeni, na hivyo kutengwa na Mungu, Kwa ujumla, mafundisho yote haya yanayotokana na Shetani, yanalenga kuwafanya watu waendelee kutenda dhambi, huku wakipuuza ukweli juu ya Jehanum, kwa kuwaza kwamba watateseka dakika chache na kupotea kabisa na ndiyo mwisho. Hiyo siyo kweli.

Ukweli kuhusu Jehanum ya moto ni upi basi? Sikiliza nikuambie! Jehanum ya moto, au Kuzimu, ni shimo kubwa na refu sana lililojaa moto. Wengi tunafahamu jinsi wanawake wanavyouchochea moto wa kuni au mkaa, kwa kuupulizia hewa kwa mdomo, au kipepeo. Sasa basi, moto wa Jehanum nao huchochewa mfululizo, ili usizimike; lakini huchochewa na pumzi ya Bwana, yaani pumzi maalum ya Mungu mwenyewe (ISAYA 14:15; 30:33). Moto wa Jehanum ni mkali sana kuliko moto wowote tunaoufahamu duniani. Moto wa gesi wa kuunganishia vyuma, unaotokana na kuwashwa mchanganyiko wa gesi ya ”Oxygen“ na ”Acetylene“, moto huu unaonekana kwa hapa duniani kwamba ni mkali. Moto huu, siyo chochote, ukilinganishwa na moto wa Jehanum. Katika karakana au viwanda vinavyotengeneza vifaa vya chuma, chuma huyeyushwa na kuwa ujiuji katika matanuru ya moto mkali unaofikia nyuzi joto 2,000 hadi 3,000 na zaidi. Moto huu unaoyeyusha vyuma na ukali wake, huo si chochote! (Kumbuka kwamba maji yaliyochemka sana hufikia nyuzi joto 100 tu!). Moto ulio katikati ya jua linalotuangaza, unafikia nyuzi joto milioni kumi . Moto wa jua nao, si chochote ukilinganishwa na moto wa Jehanum! Ukali wa moto wa Jehanum, unatisha (WAEBRANIA 10:26-27). Siyo hilo tu, moto wa duniani una rangi mbalimbali, njano, bluu, nyekundu n.k. Moto wa Jehanumu ni tofauti kabisa; Ni moto wa rangi nyeusi, unaosababisha giza na kumfanya mtu aliye motoni, awaone wenzake wachache tu wa karibu naye, hivyo hamna faraja ya kusema ”tuko wengi!“ Moto huu mweusi, ndiyo maana unaitwa ”giza la nje“ Mathayo 8:11-12, 22:13; 25:30; YUDA 1:6). Siyo hilo tu. Moto huu wa Jehanum, una meno! Hivyo una uwezo wa kuwala na kuwatafuna walioko motoni (KUMBUKUMBU 32:22; WAEBRANIA 10:26-27). Hata hivyo, pamoja na moto huu kumtafuna mtu, bado una sifa ya kumhifadhi mtu huyo na kumfanya asimalizike, kama jinsi chumvi ilivyo na uwezo wa kuizuia nyama kuharibika. Hivyo moto unamtafuna mtu wakati wote, lakini haishi na wala moto wenyewe hauzimiki. Ndiyo maana unaitwa moto wa milele (MARKO 9:43-49; MATHAYO 25:41).

Moto huu wa Jehanum, huambatana na madini yanayoitwa kiberiti au kwa lugha ya kitaaluma, Sulphur.“ Kwa wale wanaofahamu kidogo somo la shule la ”Kemia,“ au ”Chemistry,“ wanafahamu kwamba madini ya ”sulphur“ yakiwashwa moto, huwa kama mpira, na hutoa harufu mbaya kama ya mayai yaliyooza. Harufu ya namna hii

inafunika kuzimu yote, na watu walioko huko wanahangaika kushika pua zao, lakini hakuna jinsi! Hebu jaribu kuwaza maisha haya, ndiyo yawe ya milele, mpendwa msomaji! Siyo hilo tu! Katika moto huu, wamo funza maalum ambao huwatafuna watu na kufanya matundu mengi makubwa katika miili yao, wakiingia na kutoka, kutoka ubavu hadi ubavu mwingine, kutoka kwenye tumbo hadi mgongoni n.k. Hii hufanya sura za wale walioko motoni, kuwa mbaya mno kama madude tu! (ISAYA 14:11; MARKO 9:43-49; ISAYA 66:24). Hata kama mtu alikuwa mweupe duniani, huko motoni, huwa ni mweusi tii!

Moto wa milele, huitwa pia mauti ya pili (UFUNUO 21:8). Kwa nini huitwa mauti ya pili? Uchungu wa mauti unaomfanya mtu kugugumia kwa mateso makali, akishindwa kupumua vizuri na kubaki kusema ”Mmh! Mmh! Mmh!, mpaka watu wanasema heri afe apumzike, uchungu wa jinsi hiyo humkabili mtu aliye motoni, milele na

milele. Kwa lugha rahisi, ni kusema kwamba watu walioko motoni, wakati wote wako katika hali ya kufa, lakini hawafi! Niseme nini ili unielewe! Watu walioko motoni, hujawa wakati wote na vilio, na tena husaga meno yao kama mtu anayeona baridi kali (MATHAYO 8:12). Walioko motoni wanajifahamu, na kuwakumbuka wenzao waliowaacha duniani, na tena wakati mwingi hutoa ndimi zao nje, kama mbwa, wakitamani maji kidogo kupoza ulimi kutokana na joto kali linalosababisha kiu kubwa, lakini hawapati maji hata tone! Juu ya yote hayo katika vilio vyao, humwomba Mungu awahurumie na kuwasamehe lakini Yeye amekwishasema, Nami jicho langu

halitaachilia, wala sitaona huruma (EZEKIELI 9:10; 8:18).

Watu walioko motoni, hutamani mtu mmoja kati yao atoke motoni aje duniani, awashuhudie ndugu zao, ili waache dhambi, na kukwepa mateso yao, lakini huambiwa kwamba ndugu zao wanapaswa kuyasikia maneno ya manabii walioko duniani, maana hata akitumwa mtu kutoka motoni na kuelezea mateso ya huko, watasema ni mwongo, hajaenda motoni. Tunasoma haya katika LUKA 16:27-31, ”Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali

hapa pa mateso. Ibrahimu akasema, wanao Musa na manabii, wawasikilize wao. Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea watu atokaye kwa wafu, watatubu. Akawaambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa (hawatashawishika) hata mtu akifufuka katika wafu.“

Mpendwa msomaji, ikiwa mama yako mzazi alifariki akiwa hajaokoka, ujue yuko motoni, na anakuambia, ”Usinifuate huku mwanangu“. Ikiwa baba yako mzazi alifariki akiwa dhambini, anateseka motoni, na hataki umfuate huko aliko! Ndugu, marafiki na jamaa zako walioko huko wanakukumbuka sana, na hawapendi ujiunge nao huko,

bali wanataka utubu na kuokoka mateso hayo ya moto. Walioko huko motoni, wakimwona yeyote mwingine kutoka duniani, ambaye alikuwa na nafasi ya kusikia habari kama hizi na akazipuuza, kisha akawafuata huko motoni, humwambia, ”Je, wewe nawe umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe umekuwa kama sisi!“(ISAYA 14:10).

Mpendwa msomaji, baada ya kusikia yote haya kutoka kwa nabii aliyetumwa kukuletea ujumbe huu, usifanye moyo wako kuwa mgumu. Hii ni nafasi ya kipekee ya kuokoka. Je, unajuaje kama utaamka kitandani baada ya kulala usiku wa leo? Wakati uliokubalika wa wokovu ni sasa (2WAKORINTHO 6:2). Labda unajiuliza, ili uokoke, ufanyeje? Jibu ni rahisi. Kwa imani ukitubu dhambi zako huku ukimaanisha kuziacha, na kumwambia Yesu Kristo akusamehe, utasamehewa sasa hivi, na msamaha wa dhambi, huambatana na wokovu (LUKA 1:77). Je, uko tayari kuokoka sasa hivi? Najua uko tayari.Basi fuatisha sala hii kwa dhati toka moyoni,



”Mungu Baba asante kwa kuniletea ujumbe huu. Natubu dhambi zangu zote, kwa kumaanisha kuziacha. Yesu Kristo nakuomba unisamehe dhambi na kuniokoa kutoka katika mateso ya moto wa milele. Asante, kwa kuniokoa, katika Jina la Yesu. Amen. Tayari sasa umeokoka, na kwa hakika utakwenda mbinguni, hata ukifa leo. Ili uzidi kuukulia wokovu, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!

Jumapili, 21 Aprili 2013

USHUHUDA WA ADELAIDA JUU YA MBINGU NA KUZIMU
Mwanamke mmoja kutoka Bolivia aitwaye Adelaida De Carrillo alipelekwa Mbinguni na Kuzimu na Yesu Kristo. Kule alionyeshwa ni Utakatifu gani anaotakiwa mtu kuwa nao ili aweze kuingia kwenye UFALME WA MUNGU, na pia ni dhambi gani (ambazo wengi wetu tunadhani kuwa ni ndogo), zinaweza kumfanya mtu aingie Jehanamu.

Tuko kwenye safari ya maisha ya kimwili h...apa duniani tukielekea kwenye maisha ya kiroho kwenye ulimwengu ule ujao. Huo ni ulimwengu halisi ambao una maisha halisi, utawala halisi na kanuni halisi za kuingia huko.

Wakati ulimwengu tuaoishi leo una serikali nyigi na watawala wengi, ulimwengu ule ujao utakuwa na serikali moja tu inayoongozwa na Yesu Kristo. Wakazi wa uliwengu huo ni watakatifu WOTE!!!

Huo ni ulimwengu unaoongozwa na Mungu mwenyewe kwa upendo na amani. Kule hakuna magonjwa, vita, njaa, na dhambi zingine zote. Tiketi ya kuingia kule ni moja tu: nayo ni kumwamini Yesu Kristo kama Mwokozi aliyekufa na kufufuka kwa ajili yetu. Kisha tunaishi hapa duniani kwa kutii maagizo yake.

Hata hivyo, wale wote ambao hawatakuwa wamestahili kuingia kwenye ulimwengu huo (kutokana na wao kuishi maisha ya dhambi na uasi dhidi ya sheria za Mungu hapa duniani), watatupwa nje ya mbingu kweny giza na moto, yaani kwenye jehanamu ya milele.

Katika ushuhuda huu, tunaona kile ambacho Bwana Yesu anatuagiza ili tuweze kustahili kuingia kwenye ufalme ule ujao na kuishi na Mungu MILELE!!!

Adelaida De Carrillo anasema:

HATUA YA 1: Ilianzia Kanisani kwenye wakati wa Huduma

Katika Ezekieli 36:25-26, Biblia inasema:
“Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.”

Ushuhuda wangu uko namna hii: Siku moja ya Jumapili, kwenye saa 3 hivi, Kanisa letu lilikuwa na kipindi cha Huduma. Mungu alikuwa akimimina baraka zake juu yetu. Mchungaji wangu aliniambia, “Adelaida, Bwana ananiambia nikupake mafuta.”

Aliweka mafuta mengi kwenye viganja vya mikono yake na akaanza kunipaka mwilini. Alinipaka masikioni, miguuni, tumboni na kwenye mwili wangu wote. Alipoweka mikono yake kwenye uso wangu, niliona mwanga mkubwa ukija kutokea juu, ukinielekea mimi. Kuanzia hapo nilipoteza fahamu na sikujua kilichokuwa kinaendelea kwangu.

HATUA YA 2: Safari Yangu Kwenda Mbinguni

Malaika walikuja na kunichukua tukaenda juu pamoja nao. Walianza kupambana na mashetani maana njia yetu ilikuwa imewekewa vizuizi. Kulikuwa na blangeti jeusi kwenye mawingu, likiwa limejaa mapepo yaliyojaribu kutuzuia kupita. Baadaye niliona mwanga mweupe kutoka Mbinguni na malaika mzuri sana akiwa na upanga wenye nuru mkononi mwake. Aliinua upanga wake na kuanza kupigana na mapepo yale ili sisi tupite. Malaika yule alionekana kama Mwana wa Mfalme. Alikuwa na bamba la dhahabu kifuani mwake na nguo nzuri sana. Nywele zake zilikuwa za rangi ya dhahabu, na uso wake ulikuwa kama miali ya mwanga. Alikuwa mzuri sana!

HATUA YA 3: Kuoshwa na Kubadilishwa Moyo Wangu

Malaika walikuja na kunichukua tukaenda juu pamoja nao. Walianza kupambana na mashetani maana njia yetu ilikuwa imewekewa vizuizi. Kulikuwa na blangeti jeusi kwenye mawingu, likiwa limejaa mapepo yaliyojaribu kutuzuia kupita. Baadaye niliona mwanga mweupe kutoka Mbinguni na malaika mzuri sana akiwa na upanga wenye nuru mkononi mwake. Aliinua upanga wake na kuanza kupigana na mapepo yale ili sisi tupite. Malaika yule alionekana kama Mwana wa Mfalme. Alikuwa na bamba la dhahabu kifuani mwake na nguo nzuri sana. Nywele zake zilikuwa za rangi ya dhahabu, na uso wake ulikuwa kama miali ya mwanga. Alikuwa mzuri sana!

Ghafla, nilisikia sauti ndani yangu, ikisema, “Nataka ufahamu kuwa nilikupa magoti hayo ili uwe mwanamke wa maombi, na si kwa ajili ya kuzungukazunguka ukifanya mambo yasiyonipendeza Mimi. Magoti haya ulipewa ili kufanya maombezi kwa ajili ya Kanisa. Ulitakiwa kulijua hilo.”

Kwa ujumla mimi nilikuwa si mwanamke wa maombi sana. Maombi yangu yalikuwa na kawaida ya kuwa mafupi sana. Lakini Bwana alitaka niwe mwombaji zaidi.

Malaika aliendelea kuosha miguu yangu, huku akiiparua, na mimi nilikuwa namlilia Mungu anihurumie kutokana na maumivu yale. Bwana akasema: “Miguu hii ulipewa ili uwe unazunguka kwenda kuhubiri Injili yangu, kueneza Neno langu na si kuzungukazunguka kwa majirani zako kupeleka umbeya, na kufanya mambo ambayo hayanipendezi Mimi. Na kwa sababu hii,” Bwana akasema, “ninasafisha miguu yako.”

Jambo hili liliendelea na lilifanyika kwa maumivu makali sana. Bwana akasema, “Hii ni muhimu sana ili uweze kuelewa mipango niliyo nayo kwa ajili yako.”

Baadaye, nilipelekwa kwenye sehemu nyingine ambako malaika wngine watatu walikuwa wananingojea. Sehemu hii ilikuwa tofauti. Niliona vitu kama mashine. Malaika wale walianza mchakato mwingine wa kusafisha macho yangu kwa kutumia aina fulani ya mafuta. Nilihisi kama vile macho yameng’olewa kutoka kwenye matundu yake. Nikasema: “Tafadhali mnihurumie. Naomba msaada. Kwa nini mnanifanyia hivi?” Ilikuwa kama vile wanakwangua macho yangu. Kitu kama samaki kilitolewa kutoka kwenye macho yangu.

Bwana akasema, “Binti yangu, nafanya hivi kwa ajili yako kwa sababu nataka ubadilike. Mambo uliyokuwa ukifanya duniani hayakuwa yakinipendeza. Sikuwa nafurahi ukiwa duniani ulipokuwa ukitazama mambo ambayo hayakunipendeza Mimi. Ulikuwa ukitazama TV” [Soap Operas] ... “Hayo hayajengi maisha yako.” ... “Sifurahii pale wanangu wanapoangalia vitu kama hivyo; vitu ambavyo havinipi utukufu.”

Nikasema, “Bwana, nisamehe. Naomba rehema zako.” Na Bwana akasema, “Katikati ya usiku kwenye saa sita, mara zote huwa uko macho ukiangalia sinema ambazo hazikujengi wewe; na nyingi ya sinema hizo zimejazwa mambo mengi yanayohusu mapenzi. Sikukupa macho hayo kwa ajili ya mambo kama hayo. Nilikupa hayo macho ili utazame mambo yale tu yanayonipa Mimi utukufu. Na kwa sababu hii ndiyo maana ninasafisha macho yako.”

Malaika waliendelea kusafisha macho yangu huku mimi nikiendelea kuomba kuhurumiwa. Baadaye macho yangu yalipakwa mafuta, na kuanzia hapo nikawa na mtazamo tofauti; macho yangu yalibadilishwa kabisa. Bwana akasema, “Usitamani waume wa watu wengine tena!” Mimi nilikuwa na kawaida ya kuvutiwa sana na wanaume wengine, na Bwana alisema kuwa mambo hayo hayampendezi.

Nitakueleza mimi nilikuwa mtu wa namna gani. Nilikuwa Mkristo duni wa kilokole ambaye alikuwa hatendi mambo sawasawa na Biblia inavyoagiza. Kila nilichofanya kilikuwa ni kutokana na matamanio yangu na njia zangu binafsi, kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu. Nakueleza haya ili uweze kurekebisha njia zako; ili roho ziweze kuokolewa. Nakueleza kuwa tamaa NI dhambi; kuangalia michezo ya kwenye TV [Soap Operas], sinema za kidunia – mambo yote haya hayampendezi Mungu.

Malaika waliendelea na mchakato wa usafishaji. Walikuwa na kijifimbo kidogo cha kioo ambacho walikiingiza moja kwa moja masikioni mwangu. Walipoanza kukwangua masikio yangu, nilihisi maumivu makali sana. Moyo wangu ulihisi maumivu haya yote. Mara maji meusi yalianza kutoka kwenye masikio yangu, na baadaye maji ya rangi ya kijivu. Niliendelea kulia.

Bwana akasema, “Binti yangu, ninasafisha masikio yako kwa sababu ulipenda sana kusikiliza mambo ambayo hayanipendezi Mimi. Ulipenda kusikiliza umbeya. Uliyatoa kabisa masikio yako kusikiliza mambo yasiyonipendeza Mimi. Baadhi ya watu wanakuja kwako kuleta umbeya na wewe ulipenda kuwasikiliza hata kama walileta umbeya dhidi ya Mchungaji wako mwenyewe. Ulipenda kuwasikiliza hao. Badala ya kumtetea Mchungaji wako na kumsahihisha mbeya huyo ili arekebishe njia zake, ulikuwa kama wao, ukifanya umbeya pamoja nao. Usisikilize umbeya tena. Mtu akija kwako na umbeya wa aina yoyote, waombe radhi, kisha ondoka mara moja bila kushiriki. Usisikilize tena mambo yasiyokujenga!”

Nikasema: “Bwana, nisamehe!” Nilijua kuwa nilikuwa nina hatia. Hakuna jambo lililofichika mbele za Mungu. Hakuna anayeweza kujificha mbele zake. Kila tunachofanya na kusema hapa duniani kimewekwa kumbukumbu Mbinguni. Kutokana na maumivu yote yale masikioni mwangu, nikasema: “Bwana, nisamehe. Naomba rehema zako.” Hatimaye masikio yangu yalipakwa mafuta na malaika.

Bwana akaniambia: “Kuanzia leo na kuendelea, utasikiliza tu mambo ambayo nimekuruhusu kusikiliza. Utafanya mambo yale tu ambayo nimekutaka ufanye; hautakuwa Adelaida wa zamani tena. Hivi sasa wewe ni mtu mpya na ni lazima uwe ni mwanamke yule ambaye ninataka uwe.”

Baada ya hapo nilipelekwa kwenye idara nyingine ambako malaika walianza kusafisha kinywa changu. Ulimi wangu ulitolewa kabisa kinywani na kuwekwa kwenye aina fulani ya sinia. Malaika alianza kusafisha ulimi wangu, na hapa tena nilihisi maumivu makali sana. Bwana akasema: “Nataka kukusafisha. Nataka kukusafisha.”

Malaika walivyokuwa wanakwangua ulimi wangu, maji meusi yalikuwa yanatoka humo, na baadaye yalitoka maji meupe. Mwishowe malaika walitumia maji matamu sana kuoshea ulimi wangu. Yalikuwa matamu mno. Hakuna kitu duniani kinachoweza kulinganishwa na utamu wa maji yale. Kisha ulimi wangu ulipakwa mafuta. Kinywa changu nacho kilipitia mchakato huohuo. Maji meusi yalitoka kwenye kinywa changu.

Bwana akasema, “Binti yangu, ninafanya hivi kwa ajili yako ili usifanye umbeya tena; ili uache kufanya mambo yasiyonipendeza; maana ulimi wako ulishiriki katika mambo mengi sana ambayo hayanipi utukufu Mimi. Ulisema uongo mwingi sana. Acha kusema uongo! Kusema uongo hakutoki kwangu. Waongo hawanipendezi Mimi. Waongo wote hawataniona Mimi. Hakuna mwongo atakayeingia kwenye Ufalme wa Mbinguni.”

Nikasema: “Bwana, nihurumie. Najua kuwa nilifanya mambo hayo yote. Nilisema uongo mara nyingi, lakini tafadhali nisamehe.” Nilisema yote haya kwa sababu ya maumivu niliyokuwa nayahisi.

Bwana akasema: “Ninafanya hivi kwa sababu ninakupenda. Ukiendelea na hali uliyokuwa nayo, nitakupoteza. Kama nisingefanya yote haya, usingebadilika kamwe. Ni lazima niokoe moyo wako na hii ndiyo sababu ya kufanya yote haya. Nakupenda, na kwa sababu nakupenda, sitaki kukupoteza.”

Bwana akasema tena: “Kama ulivyo wewe, wengi kati ya watu wangu wako namna hiyohiyo.Wanasema uongo, wanaishi maisha ya aina mbilimbili, na wanaonekana wako safi mbele ya watu wengine. Unapomwinulia mumeo sauti ulimi wako unakuwa unatumiwa pia.” Kinywa changu kilitakaswa kabisa. Halafu Bwana akaniambia nimeze maji hayo. Nami nikafanya hivyo.

Ulimi wangu na kinywa changu vilipakwa mafuta ya thamani sana ya mbinguni. Mafuta hayo yalikuwa maalum sana, yakiwa na harufu ya thamani sana. Hayawezi kulinganishwa na mafuta yoyote ya hapa duniani. Ulimi wangu ulirudishwa tena kinywani mwangu. Malaika mmoja alikuja na kuweka hatamu kwenye koo langu. Na Bwana akaniambia: “Hii ni sawa na vile farasi anavyowekewa hatamu.”

Nikwambie tu kwamba, hii ndiyo njia pekee tunayoweza kubadilishwa. Acha kuongea maneno machafu na kushiriki katika mambo ambayo hayatujengi. Mambo haya hayampendezi Mungu kamwe.

Acha kutamka maneno machafu na yasiyo na maana. Wako Wakristo wengi – akina kaka, dada, Wainjilisti, Wamisionari, n.k., ambao wanapenda kusema maneno machafu na yasiyo na maana. Niko hapa kukuhakikishia juu ya kile ambacho Bwana alinionyesha ili maisha yako yabadilishwe. Ushuhuda huu ni kwa ajili ya wewe kubadilika. Upendo wa Mungu na wa kwangu kwako ndio ulioleta ushuhuda huu.

Ulimi wangu ulirudishiwa tena mahali pake na malaika na ukawa umebadilishwa kabisa. Naweza kukuambia sasa, hakuna mtu anayeweza kunikasirisha tena. Sasa naweza kufanya yale tu yanayompendeza Mungu.

Kisha, pua yangu nayo ilipitia mchakato huohuo. Maji meusi yalitoka puani mwangu wakati wa kusafishwa na baadaye maji meupe. Pua yangu ilipakwa mafuta na nilihisi maumivu makali sana wakati wa mchakato wa kusafishwa. Nilisema: “Bwana, tafadhali niambie mambo niliyofanya kwa kutumia pua yangu ambayo hayakukupendeza.”

Bwana akaniambia: “Baadhi ya wateja wako huvuta sigara na wewe unavuta ule moshi kupitia pua zako maana uliwahi kuwa mvutaji sigara na sasa wewe unajisikia vizuri kukaa nao wakati wanapovuta.” Nikasema: “Bwana, najua. Nisamehe. Naomba unirehemu.”

Bwana akaniambia: “Uko sawa tu na wale wote wanaovuta sigara na wote wanaokunywa pombe pale unapokaa nao na kuvuta harufu ya sigara na pombe.”

Bwana akasema tena: “Hii ndiyo sababu yangu ya kukusafisha wewe. Kwa hiyo, kuanzia leo kila utakapomwona mtu anavuta sigara au anakunywa pombe, hautajisikia vizuri kukaa nao tena. Utajisikia kinyaa.”

Hakuna cha kujitetea mbele za Bwana. Mungu anafahamu fika wewe ni nani na mimi ni nani. Libarikiwe Jina Takatifu la Bwana, Amina.

Niliendelea kumwomba Bwana rehema na nilipelekwa sehemu nyingine. Pale, malaika walianza kuosha mwili wangu uliobakia kwa kutumia sabuni nyeupe. Maji ya kijivu yalitoka kwenye mwili wangu.

Nikasema: “Bwana, nisaidie. Tafadhali, nisaidie.” Malaika walikuwa wanasugua mwili wangu na ngozi ya juu iliondoka. Damu ilikuwa inachuruzika kutoka kwenye ngozi yangu na nikamwuliza Bwana: “Kwa nini unanifanyia hivi?”

Bwana akaniambia: “Ninakusafisha. Ni lazima uwe safi mwili wako wote, nafsi yako, na roho yako. Roho yako, nafsi na mwili ni lazima viwe safi, asema Bwana.”

Sabuni ilisuuzwa kutoka kwenye ngozi yangu kwa kutumia maji ya thamani sana. Kisha malaika walipaka mafuta kila sehemu ya mwili wangu; kila sehemu ya mwili wangu. Sehemu zote za mwili wangu zilipakwa mafuta.

Bwana akaniambia: “Usirudi tena kwenye njia zako za zamani, binti yangu. Hivi sasa wewe ni Mtakatifu wangu aliyepakwa mafuta.”

Nikasema: “Bwana, nisamehe kwa mambo yote niliyokuwa nikifanya zamani hata mbele za uwepo wako. Nisamehe Bwana kwa kuwa kila kitu ambacho Mchungaji wangu alijaribu kunisahihisha mimi nilikuwa nikipingana naye. Nilisema mambo mengi kwake ambayo sikutakiwa kusema.”

Mchungaji wangu mara nyingi alikuwa akiniambia kuwa mavazi yangu kama Mkristo hayakuwa sawa. Nilishindana naye sana. Aliwahi kuniambia kuwa nilisema uongo na mimi nikahuzunika. Pale mtu anapopotoka na Mchungaji wake akamsahihisha, mtu huyo huhuzunika. Siku zote mimi nilikuwa kinyume na Mchungaji wangu.

Kisha nilipelekwa kwenye idara nyingine ambako nilipokelewa na malaika watatu. Malaika wale walitumia nguo nyeupe kufuta maji kwenye mwili wangu. Kwenye nyuso za malaika wale, niliona kuwa walikuwa wanajisikia huruma sana kwa ajili yangu kutokana na yote niliyopitia lakini hawakusema kitu chochote, hata neno moja. Sikuweza kumwona Bwana kwenye sehemu hizi. Nilikuwa nasikia tu sauti yake.

Malaika wengine watatu walinipokea kwenye idara nyingine. Malaika hawa walinivika nguo nyeupe ya juu na sketi ndefu. Sketi ilikuwa ndefu sana kiasi kwamba miguu yangu ilikuwa haionekani.

Je, Baada ya Kuvishwa nguo hizo alikwenda wapi, na pengine alikuwa na nani?

*****inaendelea sehemu ya Pili*****

Jumamosi, 20 Aprili 2013

SABABU SABA ZA KIBIBLIA KWA NINI WATU WANAKUFA MAPEMA

 
Bwana Yesu asifiwe sana wana wa Mungu, ni matumaini yangu na Imani yangu ya kwamba u mzima na ya kuwa unaendelea kuufurahia uzuri wa Yesu Kristo na kazi yake ya msalaba.
Leo ninataka kwa pamoja tuyachunguze maandiko na tuzipitie sababu hizi saba za Kibiblia ni kwa nini watu wengi wanakufa mapema...na sasa ongezeko la vifo vya mapema ni kubwa kuliko hata zamani. Kwa Tanzania wastani wa kiwango cha maisha ni miaka 45,Binafsi nauona umri huu kuwa ni mdogo sana kwa mtu wa rika hili kuondoka duniani kwani anakuwa na majukumu mengi ya kufanya na pia mchango wake unakuwa unahitajika kwenye familia, ukoo, wilaya, mkoa, taifa na hata duniani kwa ujumla.
Ni maombi yangu na dua yangu kwa Bwana ya kwamba umalizapo kusoma ujumbe huu, macho yako ya ndani yatafunguka na utaweza kuona swala hili kwa jicho la Rohoni...KARIBU SANA.
               Zifuatazo ni sababu saba kwa mujibu wa Neno la Mungu ni kwanini watu wanakufa mapema(katika umri mdogo)

1.KUTOWAHESHIMU WAZAZI(BABA NA MAMA)
Biblia iko wazi sana na imesisitiza uhusiano mzuri na wa uhakika kati yetu na wazazi wetu...kinyume chake LAANA zitayaandama maisha yetu na maisha yetu hayatakuwa ya heri na marefu.
Ukisoma Waefeso 6:1-3 inasema, "Enyi watoto watiini WAZAZI wenu katika BWANA, maana hii ndiyo HAKI.Waheshimu baba na mama yako, amri hii ndiyo ya kwanza YENYE AHADI (za ustawi, baraka na wingi wa miaka), upate HERI, UKAE SIKU NYINGI( UISHI SIKU NYINGI) katika dunia"   pia katika Kumbukumbu la Torati 5:16 Biblia inasema, "Waheshimu BABA na MAMA yako; kama BWANA, Mungu wako alivyoamuru, SIKU ZAKO ZIPATE KUZIDI, nawe upate KUFANIKIWA katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako"
Kwa mujibu wa maneno ya Mungu hapo juu ni dhahiri kabisa ya kuwa watu wote wasiowaheshimu wazazi wao, ni ngumu kufanikiwa, Laana zinawafuatilia na zaidi ya yote wana muda mchache wa kuishi...WANAKUFA MAPEMA!

2.KUKOSA MAONO
  Kwa mujibu wa Biblia, mtu anayeishi ili mradi tu, asiyejua kwanini yupo duniani, asiyekuwa na kusudi na mpango katika maisha yake, na asiyeweza kupanga hata mipango ya 'kesho nitafanya a, b, c nk' yuko katika hatari kubwa ya kuondoka duniani kabla ya muda wake...Biblia inasema, "Pasipo MAONO watu huangamia"....Biblia ya kiingereza inasema, "Without VISION people PERISH"
Jitahidi kuwa na maono ya muda mfupi na ya muda mrefu, Mungu anashughulika na walio nacho, wasiokuwa nacho hata kile kidogo walichonacho hunyang'anywa.

3.KUTOKUMCHA MUNGU
Kumcha Mungu ni kuishi maisha yanayoongozwa na HOFU ya MUNGU (si woga dhidi ya Mungu)...Ni maisha ambayo moyo,mwili, nafsi na roho ya mtu inakuwa imejawa na kiu na njaa ya kumpendeza Mungu na kuyafanya maagizo yake yote-tena kwa furaha.
Mithali 10:27 inasema, "KUMCHA BWANA kwaongeza siku za mtu, Bali miaka yao WASIO HAKI itapunguzwa"  na pia Mhubiri 7:17 inasema, "Usiwe MWOVU kupita kiasi; wala usiwe mpumbavu; kwanini UFE KABLA YA WAKATI WAKO?"
Kwa mujibu wa ushahidi huu wa Neno la Mungu, ni dhahiri kuwa maisha yasiyo na uchaji na yasiyoongozwa na hofu ya Mungu, yanawafanya wengi wafe kabla ya muda wao waliokusudiwa kuishi.

4.KUMWEKEA MUNGU MIPAKA
Hii ni hali ya mwanadamu kuamini kuwa Mungu anaweza hili na hili hawezi...kitendo hiki Mungu anakiita kuwa ni 'DHARAU' kwake... Zaburi 78:41 inasema, "Wakarudi nyuma wakamjaribu MUNGU; Wakamwekea MPAKA Mtakatifu wa Israel"
Mstari huu wa Zaburi unaelezea maisha ya wana wa Israel njiani toka Misri kwenda nchi ya Maziwa na Asali-Kanaani.
Biblia inaeleza jinsi Musa alivyowatuma wapelelezi 12 kwenda kuipeleleza nchi ya ahadi waone kama kama kweli ni nchi ya 'Maziwa na Asali'...10 kati yao Waliporudi walirudisha ripoti ya kuwa kweli ile nchi ni ya maziwa na asali, ila inakaliwa na Wanefili-wana wa Anaki...majitu na ya kwamba wao ni kama panzi tu na hawawezi kwenda na kuimiliki. Joshua na Kalebu walileta habari njema...waliona kwa macho lakini wakazungumza kile ambacho ni 'UHAKIKA WA MAMBO YATARAJIWAYO' wakamwamini Mungu kuwa aweza kuwapa ile nchi kuwa milki yao sawa na alivyomwapia Ibrahim(Hesabu sura ya 13 na ya 14) na wote waliomwekea Mungu mpaka walikufa huko jangwani, hawakuingia nchi ya ahadi...WALIFUPISHA MAISHA YAO KWA KUTOKUAMINI KWAO...Ila Kalebu aliishi muda mrefu sana, alikuwa na nguvu kama za mtu wa miaka 40 hata alipokuwa na miaka 85( soma Joshua 14:6-14) na inaeleza pia ya kuwa Joshua alikuwa MZEE SANA, alikufa akiwa na miaka 110 lakini alikuwa na nguvu zake kamili mpaka pale BWANA alipompumzisha(Joshua24:1-29)
Kama unataka kuwa na maisha marefu, na unataka kuziongeza siku zako...ishi maisha ya IMANI...Usimwekee Mungu mipaka, kumbuka, "Njia zake zi juu mno na fahamu zake pia" Isaya 55:8-11

5.KUTOKUMTUMIKIA MUNGU
Biblia inasema katika KUTOKA 23:25-26, " Nanyi  mtamtumikia BWANA, Mungu wenu naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; NAMI nitakuondolea Ugonjwa kati yako...na  hesabu ya SIKU zako nitaitimiza"
Huu ni ukweli ambao inabidi uufahamu na uweke kwenye matendo.Unataka kuishi muda mrefu hapa duniani? kazi ni rahisi...fanya sehemu yako, MTUMIKIE BWANA naye ATAITIMIZA hesabu ya siku zako...HAUTAKUFA KABLA YA WAKATI.

6.MAISHA YA DHAMBI
Dhambi ni mbaya...inakutenga mbali na Mungu( Isaya 59:1-2) lakini kibaya zaidi inapunguza maisha yako...inakufanya ufe kabla ya muda wako...Unafurahia kuishi maisha ya dhambi? ni mzinzi, mwongo, msengenyaji, usiyesamehe,mwenye kinyongo, kisasi nk? Unajipeleka kaburini kabla ya wakati wako...unafanya kazi ambayo mshahara uitwao 'MAUTI' utaupata.
Katika Warumi 6:23 Biblia inasema, "Kwa maana mshahara wa DHAMBI ni MAUTI(KIFO), bali karama ya Mungu ni uzima wa Milele katika Kristo Yesu Bwana wetu"  pia Biblia inasema, "Roho itendayo DHAMBI ndiyo itakayokufa"
Maisha ya dhambi yanakata muda wa mtu wa kuishi...Ni wangapi waliokufa wakiwa vijana wadogo kwa sababu ya UKIMWI kwa kutoikwepa dhambi ya Uzinzi? au ni Wezi wangapi wamekufa wakiwa katika harakati za kuiba?
Dhambi ni adui mkubwa kwangu na kwako!

7.KUKOSA BIDII KATIKA KUMPENDA MUNGU
Biblia iko wazi katika Zaburi ya 91:14-16, nayo inasema, "Kwakuwa AMEKAZA(Ameweka bidii katika) KUNIPENDA, Nitamwokoa; na kumweka palipo juu (NITAMWINUA) kwa kuwa amenijua Jina langu. Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni. Nitamwokoa na kumtukuza; KWA SIKU NYINGI nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu"
Biblia inasema Atakayekaza/kuwa na bidii katika KUMPENDA MUNGU atashibishwa kwa WINGI WA SIKU.
Yesu ameweka wazi ni namna gani waweza kumpenda Yeye, Yohana 14:21 inasema, "Yeye aliye na AMRI  zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye, naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; Nami nitampenda na kujidhihirisha kwake"
Nayo Mithali 3:1-2 inasema, " Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike AMRI zangu.Maana zitakuongezea WINGI WA SIKU, NA MIAKA YA UZIMA, NA AMANI"
Unapozishika sheria na Amri alizozitoa Bwana maishani mwako...huo ndo udhihirisho wa Upendo wako kwa Mungu aliye hai...kila unapoongeza bidii ya kumtii na kumheshimu Mungu-ukakaza kumpenda, ANAKUSHIBISHA KWA SIKU NYINGI...Wewe ndiye unayeweza kumwambia Bwana, hii miaka 90 inatosha, nimekwisha shiba maisha...nataka kurudi nyumbani...au miaka 40 inatosha Bwana...nimeshiba siku nataka kurudi nikae na wewe...wewe ndo unayeamua wingi wa siku zako...tangu leo kaza kumpenda BWANA.

              Ninaamini umejifunza kitu, na ya kuwa wewe nawe utayagusa maisha ya wengine kwa KWELI hizi ambazo Bwana amesema na wewe kupitia kwangu.Ubarikiwe
   Wako katika na Ndani ya Kristo

Jumatatu, 15 Aprili 2013

UONGOZI WA KIROHO


SEHEMU I

  1. UTANGULIZI
Uongozi na Kiongozi. Nini tofauti yake?.

- Uongozi ni tendo la kuongoza, hali ya kutangulia mbele au kuelekeza watu njia au mwelekeo wa kuendea jambo au kufikia malengo fulani.

- Kiongozi ni mtu yule ajuaye njia au mwelekeo wa jambo hilo au malengo hayo na ana uwezo wa kuwatangulia na kuwavuta wengine wamfuate.

Musa – Kut. 10:25,26, Kut. 13:21,22,
Yuda – Mwa. 46:28,
Yesu – Yoh. 14:6, 10:2-4,
Paulo - 1Kor. 11:1, 4:16.

Kwa nini viongozi wanahitajika?

Hitaji kubwa la nyakati zote katika watu wa kada zote, jamaa, taifa na mataifa, taasisi na mashirika ya dini ni kupata viongozi wenye sifa na uwezo wa kuwaongoza. Wenye uwezo na hekima katika kuwaunganisha watu ili kuwafanya kuwa wamoja katika kutumia karama, vipawa na talanta au rasilimali walizo nazo kwa manufaa ya maendeleo yao, pia waweze kufikia na kulikamilisha jambo au malengo na mipango yao waliyokusudia. Viongozi wanajua wanalopaswa kulifanya na wana uwezo wa kuwachukua watu mbele zaidi ya pale walipo sasa.

  1. TOFAUTI YA KIONGOZI WA KIROHO NA WA KIDUNIA

Uongozi wa kiroho na ule wa kidunia unaweza ukafanana katika baadhi ya mambo fulani tu, lakini ukatofautiana sana na kwa kiasi kikubwa katika mambo ya kimsingi. Kwa mfano katika mambo yafuatayo:-

i). Hitaji na maandalio ya kiongozi: Mungu huandaa na kuweka Viongozi.

1Sam. 16:3,7 “Umwite Yese, nami nitakuonyesha utakayotenda, nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako…Bwana akamwambia Samweli, usimtazame uso wake wala erefu wa kimo chake, .. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo, maana binadamu huangalia sura ya mtu, bali Bwana huangalia moyo”. (Eze. 16:1-5, 1Tim. 3:1,15)

Yer. 3:15. “Nami nitawapa ninyi wachungaji wanipendezao moyo wangu, watakaowalisha kwa maarifa na ufahamu”.

Mat. 9:38 “Basi, mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake”.

ii). Nia ya ndani ya Kiongozi:

- Kwa nini wewe ni kiongozi au unataka kuwa kiongozi?
Zipo nia mbalimbali kama vile kutaka mamlaka, sifa, kuheshimiwa, utukufu, kutosheka, kushika hatamu, utajiri, kutambulika, kiburi, nafasi nzuri nk. Ambazo hizo ni nia za viongozi wa kidunia.

- Na pia mtu anaweza kuwa kiongozi kwa nia ya kutaka kuyafanya mapenzi ya Mungu.
- Flp. 2:5,13 “Iweni na nia iyohiyo ndani yenu ambayo iliyokuwamo pia ndani ya Kristo Yesu.. maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.”

- Uongozi wa kidunia unadhihirishwa katika nia binafsi katika kupata mafao yenye kumnufaisha yeye na familia yake, kupata malupulupu mazuri yenye kuinua heshima yake bila kujali wengine kama wanaumia au la. Hivyo watu wanapigania kuwa viongozi kwa nia ya cheo, na kuona umuhimu zaidi kuliko huduma yenyewe itakayotolewa au utendaji / uongozi wa kazi yake kwa watu.

- Uongozi wa kiroho, Mungu anasema “Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno, bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mabo ya wengine.” (Flp. 2:3,4)

iii). Kutaka mapenzi ya Mungu:

- Rum. 12:2. “…msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwe na kufanywa upya nia zenu na kujua hakika mapenzi ya Mungu.” (Efe. 5:17)

- 1Tim.3:1. “Ni Neno la kuaminiwa, mtu atakaye kazi ya askofu, atamani kazi njema”. Tunaona Mungu hamkatai mtu yeyote kuhitaji kuwa kiongozi, anatamani kazi njema. Lakini nini hasa nia yake ya moyoni? Hilo ndilo litakalombainisha kama atakuwa kiongozi wa kiroho au wa kidunia.

- Kiongozi wa kiroho, yeye ni kiungo au mpatanishi kati ya Mungu na watu anaowaongoza.

Mfano:

Musa: Kut. 19:9, 24:3. “Bwana akamwambia Musa, Mimi naja kwako katika wingu zito, ili watu hawa wasikie nitakaposema nawe, nao wapate kukuamini wewe nawe hata milele. Musa akamwambia Bwana hayo maneno ya watu. …. Musa akaenda akawaambia watu maneno yote ya Bwana, na hukumu zake zote, watu wote wakajibu kwa sauti moja, wakasema, Maneno yote aliyoyasema Bwana tutayatenda.”

Yesu: Yoh. 8:26-30. “Ninayo mengi ya kusema na kuhukumu juu yenu, lakini yeye aliyenipeleka ni kweli, nami niliyoyasikia kwake ndiyo ninenayo katika ulimwengu… sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha, ndivyo ninenavyo. Naye aaliyenipeleka yu pamoja nami, hakuniacha peke yangu, kwa sababu nafanya siku zote yale yampendezayo. Na alipokuwa akisema hayo wengi wakamwamini.”

Paulo: 2Kor. 5:18-20. “Lakini vyote vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho… ametia ndani yetu neno la upatanisho… Basi tu kwa ajili ya Kristo…twawaomba ninyi mpatanishwe na Mungu.”







SEHEMU II


3. UMUHIMU WA UONGOZI

Uongozi tunaona ni muhimu sana mbele za Mungu na kwa watu pia. Uongozi ni kipawa cha Mungu kwa wanadamu ili wakae katika amani na matumaini. Bila uongozi watu hukosa mwelekeo na amani, hivyo kusababisha watu kufikia hatua ya kufarakana, kutawanyika kukosa mwelekeo, kila mtu kwenda au kutenda lile analoona linamfaa yeye machoni pake. Kwa sababu hiyo Mungu ameweka uongozi ili watu wapate mwelekeo, amani na matumani katika kuyatimiza mapenzi yake duniani. Tunasoma katika Biblia kuwa:

Amu. 21:25: “Siku hizo hapakuwa na mfalme katika Israeli, kila mtu allifanya yaliyokuwa mema machoni pake mwenyewe.”

Zek. 13:7: “…Mpige mchungaji, nao kondoo watatawanyika..”

Hes. 27:15-23: “Musa akanena na Bwana akisema; Bwana Mungu wa roho za wenye mwili wote, na aweke mtu juu ya mkutano, atakayetoka mbele yao, atakayewaongoza watokapo, na kuwaleta ndani; ili mkutano wa Bwana usiwe kama kondoo wasio na mchungaji.”

Efe. 4:11-13: “Naye alitoa wengine kuwa Manabii, na wengine kuwa Mitume, na wengine kuwa Wainjilisti, na wengine kuwa Wachungaji na Waalimu. Kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe, hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani, na kumfahamu sana mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo ha utimilifu wa Kristo. Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, na hila ya watu, kwa ujanja tukizifuata jia za udanganyifu”.


4. SURA YA UONGOZI WA KIROHO

Mambo matatu yanayotakiwa kuonekana ndani ya uongozi wa kiroho ni kama yafuatayo:-

i) Utumishi
ii) Uchungaji
iii) Uwakili

i) UTUMISHI

Mk. 10:45, Lk. 22:24-27, Mat. 20:26-28, Yoh. 13:17.

a) Je, wewe ni kiongozi wa aina gani?

- Mimi ni kiongozi ninayeongoza.
- Mimi ni mtumishi ninayetumika.
- Mimi ni kiongozi mtumishi.
- Mimi ni mtumishi kiongozi.

b) Mtumishi kiongozi - hii ni filosofia inayowasaidia watu kuwa na dhana ya utumishi; na baadaye kuweza kuongoza kwa nia kuwatumikia watu, shirika au kanisa. Mtumishi kiongozi anaweza asiwe na cheo chochote kanisani na bado akawa tegemeo la watu wengi, kutoka kwake, watu wanapokea hazina njema kutoka kwake kwa jinsi anavyowatumikia na kuwaongoza kwa namna moja au nyingine.

Neno la Mungu linatuonyesha maneno ya msingi na yenye hekima katika utumishi kama yafuatayo:-

Lk. 22:26,27: “Lakini kwenu ninyi sivyo; bali aliye mkubwa kwenu na awe kama aliye mdogo, na mwenye kuongoza kama yule atumikaye..Lakini mimi (Yesu) kati yenu ni kama atumikaye”.

Mat. 20:26-28: “..Bali mtu yeyote atakaye kuwa mkubwa kwenu na awe mtumishi wa wote; na mtu atakayekuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; kama vile mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi”.

1Pet. 5:2,3: “Wala si kama wajifanyao mabwana katika mitaa yao; bali kwa kujifanya kielelezo kwa lile kundi”.

c) Tabia ya Mtumishi kiongozi:-
- Mnyenyekevu. (Mat. 10:24, 2Tim. 2:25)
- Ana bidii si mvivu. (Mat. 24:45-47)
- Ana uwezo wa kufundisha. (2Tim. 2:24)
- Mvumilivu. (2Tim. 4:2)
- Mtii. (Ef. 6:5,6, Tito 2:9)
- Amejitoa. (2Sam. 15:21)
- Mwangalifu. (Lk. 12:35,36)
- Mwaminifu. (1Sam. 22:14)
- Amejaa Roho Mtakatifu. (Mdo. 2:16,18)

ii) UCHUNGAJI
Zab. 23, Yoh. 10:11, 21:15-17, 1Pet. 5:2-3.

a) Kiini cha uchungaji
- Neno mchungaji lilitumika sawa na mchungaji wa kondoo, n’gombe au mifugo mingine. (Yer. 6:3, Mat. 8:33)
- Mchungaji hukaa na kondoo na kazi yake muhimu ni kuwa na kondoo hizo.
- Kondoo ndiyo wanampa kazi ya kuwa mchungaji, hivyo mchungaji ni mtumishi wa kondoo.

b) Sifa ya mchungaji
- Mchungaji anawajua kondoo wake kwa majina. (Yoh. 10:3,14,27). Sawa na Haruni juu ya wana wa Israeli. (Kut. 28:9,10,12,29)
- Mchungaji yuko pamoja na kondoo au anapatikana na ni rahisi kuingilika. (Lk. 22:27)
- Mchungaji anatangulia mbele kuwaonyesha kondoo mahali pa malisho, majani na maji. (Zab. 23:1,2)
- Mjasiri na yuko tayari kujitoa kwa ajili ya kondoo. (Yoh. 10:10-18)
- Anawaongoza na kuwaelekeza kwa upole kwa fimbo ya kichungaji. (Zab. 23:4, Ufu. 21:15)

c) Ili kutimiza wajibu wake kwa kondoo
Mchungaji anapaswa kujua mambo matatu.
- Kwamba ameitwa na Mungu. (Yoh. 15:16)
- Kufahamu chanzo cha nguvu zake. (Kol. 1:11,29, Zek. 4:6)
- Kufahamu mambo aliyoitiwa kufanya, na hata jinsi ya kuyapatia vipao mbele. (Yoh. 10:4)

Mambo hayo humfanya mchungaji kuwa na maono, malengo na mipango katika kazi yake. (Kol. 1:10, Efe. 4:1)

d) Mchungaji anapaswa kuhakikisha kuwa kundi lake
- Linaongezeka kiidadi. (Mdo. 2:47, 41, 6:7)
- Linakua kiroho. (Mdo. 2:42, 2Kor. 2:14, Kol. 1:10)
- Linamwabudu Mungu katika Roho na kweli. (Yoh. 4:24, 2Kor. 4:2)
- Linahifadhi umoja na ushirika katika mwili wa Kristo. (Fil. 1:27, Efe. 4:1-6)
- Linaushuhudia ulimwengu habari njema na kuwaleta kwa Kristo. (Mdo. 5:42, 6:7)
- Linapata ulinzi au usalama na amani. (Mdo. 20:28-31)

e) Tahadhali za mchungaji kama kuhani wa Mungu ni kuona kuwa:-
- Katika uongozi wake asiwe sababisho la kundi kutawanyika.
- Yer. 23:1,2: “Ole wao wachungaji, wanaoharibu kondoo za malisho yangu na kuwatawanya! Asema Bwana… Mungu asema hivi, juu ya wachungaji wanaowalisha watu wangu. Mmetawanya kundi langu na kuwafukuza, wala hamkuenda kuwatazama, angalieni, nitawapatiliza uovu wa matendo yenu, asema Bwana”.

- Eze. 34:2-5,10: “Ole wao wachungaji wanaojilisha wenyewe, je haimpasi mchungaji kulisha kondoo? Mnawala walionona, mmejivika manyoya, mnawachinja walionona lakini hamwalishi kondoo. Wagonjwa hamkuwatia nguvu, wala hamkuwaponya wenye maradhi, wala hamkuwafunga waliovunjika, wala hamkuwarudisha waliofukuzwa, wala hamkuwatafuta waliopotea, bali kwa nguvu na kwa ukali mmewatawala. Nao wakatawanyika kwa sababu hapakuwa na mchungaji, wakawa chakula cha mbwa-mwitu, wakatawanyika.”

- Hapotoshi mafundisho ya kweli, yaani hafundishi kwa nia ya kulidanganya kundi kwa manufaa yake binafsi.

- Eze. 22:26,30: “Makuhani wake wameihalifu sheria yangu, wametia unajisi vitu vyangu vitakatifu; hawakuweka tofauti kati ya vitu vitakatifu na vitu vya kutumiwa siku zote; wala hawakuwafundisha watu kupambanua vitu viichafu na vitu visafi, nao wamefumba macho yao.. Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.”

- Tito 2:7,8: “Katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu, na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa..” (Eze. 13:1-7, Isa. 10:1-3, Yer. 14:14)

- Anatoa malisho kwa kundi kama Mungu anavyokusudia na kwa wakati unaokubalika.

- Yer. 23:22: “Lakini kama wangalisimama katika baraza yangu,ndipo wangaliwasikizisha watu maneno yangu, na kuwageuza waziache njia zao mbaya na uovu wa matendo yao.”

- Mat. 24:45,46: “Ni nani basi, mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? Heri mtumwa yule ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo”.

- 2Tim. 2:15 “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli”. (2Tim. 4:5)

- Kwa kufanikisha haya mchungaji lazima anazingatie Maombi na kusoma Neno la Mungu kila wakati.

- Mat. 17:20,21: “Kwa maana amini nawaambia, mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu. Ondoka hapa uende kule, nao utaondoka, wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga”.

- Yoh. 15:7: “Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu. Ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa” (Fil. 4:6, 1The. 5:17, Kol. 3:16, Yoh. 17:14-17)

iii) UWAKILI

Mat. 25:14, 1Kor. 4:1,2.

- Katika Agano jipya, wakili alikuwa ni mtu aliyeaminiwa na bwana wake; na hivyo alipewa mafao na mamlaka na pia alikuwa na wajibu na uajibikaji kwa kazi yake. (Lk. 12:42-43)

- Wakili alipaswa kuangalia vipawa katika maisha ya wale anaowangoza ili avitumie vizuri na kuzalisha. (2Tim. 1:14, 1Tim. 1:18-20)

- Wakili anapaswa kuhesabu rasilimali zote alizonazo, kama vile, watu, fedha, vifaa na kwa neema ya Mungu kuweza kupanga na kuvitumia ipasavyo.

- Wakili anapaswa kuwa mkweli (honesty), mwenye msimamo mwema (integrity) na muwazi (transparency). (Yoh. 8:12)

- Mtu mwaminifu na mwenye kupandishwa daraja kwa uaminifu wake. (Mat. 25:21) ”Bwana wake akamwambia,Vema mtumwa mwema na uaminifu, ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi…”

1Kor. 4:1,2: “Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu” (Mat. 24:45-47)







SEHEMU III




5. MAADILI YA KIONGOZI WA KIROHO

Maadili ni jambo linaloweza kutenganisha sifa za uongozi katika muonekano wake kati ya uongozi wa kiroho, na wale uongozi wa kidunia. Maadili yapo hasa kuonyesha msimamo katika usafi wa maisha na haki.


Mtume Paulo katika 1Kor. 10:23, 6:12 anasema:
Vitu vyote ni halali, bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo. …. lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu chochote.”

Vipi yale mambo yanayokupa msukumo zaidi na yale unayoyapendelea kuyafanya, licha ya kuwa unayofanya yanamkosea Mungu? Na pengine yamekuwa kikwazo hata kwa wale unaowaongoza! Unajionaje mbele za Mungu, je, ni sawa au si sawa?

- Katika waraka wa kwanza kwa Timotheo 3:2-12. Neno la Mungu limeeleza maadili ya msingi kwa kiongozi wa kiroho ya kuwa anapaswa awe mtu wa: - kutokulaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtaratibu, mkarimu, mwenye kujua kufundisha, si mlevi, si mpiga watu, si mtu wa majadiliano, si mpenda fedha, mwenye kusimamia nyumba yake, si mchanga kiroho, mwenye kushuhudiwa na walio nje. Si mwenye kauli mbili, asiyetamani fedha ya aibu. (Tito 1:6,7)

- Maadili yanatusaidia kuishi maisha ya mfano au kielelezo.
Katika Tito 1:8,9 tunasoma kiongozi awe “Mkaribishaji, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kudhibiti nafsi yake, akilishika lile neno la imani vile vile kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima na kuwashinda wenye kupinga.”

(2Thes. 3:9, 1Tim. 4:12, 1Sam. 12:2-5)
- Unayoyafanya yatageuza watu zaidi ya yale unayoyasema.
- Unavyoishi itasaidia kukazia mafundisho yako au pia kuyaondoa kabisa mioyoni mwa watu wanaokutazama.
- Kumbuka kuwa watu hujifunza zaidi kwa kuona, kisha kwa kusikia na kwa kiasi kidogo kwa yale mengineyo.
- Maadili bora ni uamuzi na misimamo inayoweza kumfanya mtu binafsi au jamii iweze kuishi maisha ya haki, utaratibu, na usafi.

Mfano wa watu wawili:-

Sauli

Yeye aliitwa na Mungu kuwa mfalme, alipakwa mafuta na kutumiwa na Mungu; lakini….
(1Sam. 13:13,14)
- Alikuwa mtu wa kutenda bila kufikiri, aliweza kutoa sadaka kinyume na utaratibu wa Mungu.
Alikuwa mtu wa kutumia mabavu, kiburi, kutotii na kupenda umaarufu.
(1Sam. 15:12-26)
Mwisho wa yote, alianguka na kukataliwa na Mungu. Alijiwekea maadili mabaya, ambayo hayakumpa Mungu utukufu.
Ndipo neno la Bwana likamjia Samweli kusema, Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme, maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya niliyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia Bwana usiku kucha”. (1Sam. 15:10,11)

Bwana akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, Ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli?

Nehemia

Katika Nehemia 5:14-19 tunaona Nehemia alionyesha msimamo wa haki, kama maadili yake binafsi.
- Alikusudia kufanya yaliyo mema na ya haki (mst.14)
- Alijitenga na watu walio wadharimu (anasema sikufanya kama maliwali walionitangulia. Mst. 15)
- Alijitoa na kukaza macho yake kwenye kazi (“maana hata kazi ya ukuta nikaishika sana”. Mst. 16)
- Nehemia pia alikuwa na uwezo wa kuwavuta wengine (nguvu ya ushawishi).
-- alitoa mali zake kusaidia wengine. (Mst. 17: “watu 150 walikula mezani pangu”)
-- alitanguliza maslahi ya wengine kwanza, badala ya faida yake. (Mst. 17-18)
-- Alionyesha kuwajibika kwa Mungu akimpa utukufu. (Mst. 19)
Nehemia 12:40,43: “Ndivyo walivyosimama mikutano yao walioshukuru nyumbani mwa Mungu, na mimi (Nehemia)… Wakatoa dhabihu nyingi siku ile, wakafurahi; kwa kuwa Mungu amewafurahisha furaha kuu; na wanawake pia na watoto wakafurahi, hata ikasikiwa mbali sana furaha hiyo ya Yerusalemu”.

Kukosa maadili mema kunajidhihirisha katika mambo yafuatayo :-
i). Maisha ya uasi kwa kiongozi kama vile wana wa Israeli. (1Kor. 10:1-5)
- Kutamani mabaya. (1Yoh. 2:15-17)
- Kuabudu sanamu
- Uasherati
- mawazo potofu,
- uhusiano mbaya wa mke na mume,
- kukosa hekima katika kushauri/kushauriwa.
- Kumjaribu Bwana
- Manun’guniko.

Anatazamiwa kiongozi ya kuwa “Alivyo kwa nje na ndivyo anatakiwa awe kwa ndani. Vile anavyokuwa madhabahuni/mbele ya watu ndivyo anatakiwa awe pia mbele ya familia yake”.

ii). Maisha mabaya katika fedha.
- Kupenda fedha. (1Tim. 6:6-10)
- Kutumia vibaya fedha za kanisa. (Fil. 4:11-12)
- Udanganyifu katika matumizi. (Mith. 15:27, Rum. 13:8)
- Kutokutoa fungu la kumi (zaka) na husababisha laana kwake yeye mwenyewe na kwa kundi lake. (Mal. 3:8,9, Ebr. 7:5,9,10)
- Uzembe wa kutolipa madeni. (Zab. 37:21, Mith. 22:7) hali hii inapozoeleka kwa kiongozi inamsababishia kutoaminiwa na kuonewa shaka.

iii). Matatizo katika ndoa. Yanaweza kusababishwa na
- Unafiki. Nje kuonekana tofauti na hali halisi ya ndani, kuficha au kufanya siri shida na matatizo ya kindoa. (Math. 23:27,28)
- Kutokutatua matatizo madogomadogo ya ndani, na hivyo kuzaa matatizo makubwa. (Lk. 16:10) “Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia, na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia” Yapasa kujiuliza. Je, una ujasiri wa kuhubiri mbele ya mkeo au mumeo na pia watoto? Kama unakosa ujasiri mbele yao, basi, kuna mambo yanahitajika ufumbuzi.
- Kuacha kutunza familia kwa kisingizio cha kutingwa na huduma. (1Tim. 5:8)

iv). Kuharibu huduma yako kwa:-
- Kupotosha Neno la Mungu, kughoshi, na bila ya kutumia kwa halali neno la kweli. (2Kor. 4:1,2, 2:17, 2Tim. 2:15)
- Kuwatumia watu kwa kujinufaisha yeye binafsi badala ya kuwajenga na kuwaimarisha katika ufalme wa Mungu.


Faida ya Maisha ya Maadili mema ya kiroho

Ili uwe kiongozi, lazima uwe na wafuasi, kuwa na wafuasi lazima wakuamini. Hivyo maadili bora, ni ya lazima; yanakuwezesha wewe kiongozi katika mambo yafuatayo:-
- Kuirithisha (influence) tabia yako kwa wale unaowaongoza. (Mat. 26:73) ”Punde kidogo,wale waliohudhuria wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika wewe u mmoja wao, kwa sababu hata usemi wako wakutambulisha” (1Tim. 4:12)
- Kutokuwa mtu wa kubadilika badilika kama kinyonga.
- Je, wewe ni yeye yule kila wakati?
- Je, jambo gani unafanya ambalo hutaki watu walijue?
- Hii ndiyo tabia yako? (1Tim. 3:8)
- Tabia yako isiyobadilika inagusa mioyo ya watu. (Ebr. 13:7)
- Dhamiria kuwa mkweli na muwazi, usitafute kuonekana mzuri, bali uwe mzuri. (Yer. 7:3-4)
- Tabia huweza kujengwa na kubomolewa katika mambo madogo. Dhamiria uaminifu katika yaliyo madogo hivyo utakuwa mwaminifu dhidi ya mambo yaliyo makubwa.
- Unaweza ukabadili matendo yako ili yafuatane na kanuni za maadili mema au unaweza ukabadili kanuni za maadili zifuatane na matendo yako. Uchaguzi ni wako!
- Dhamiria kuwa na nia ya kutumika kwa unyenyekevu, watu watakufuata wakijua nia na lengo lako ni kuwatumikia.

Changamoto
- Hitaji kubwa la kanisa ni kupata viongozi bora, watakaoweza kukabiliana na changamoto zilizopo nyakati hizi za mwisho katika kumwakilisha Kristo. Je, wewe ni miungoni mwao? (1Tim. 3:1-7)
- Utafanya nini wewe binafsi ili kuboresha uongozi wako?


6. MAFAO, GHARAMA NA ANASA ZA UONGOZI

Uongozi una mafao, gharama na anasa zake, anasa ni pamoja na vikwazo vilivyomo.

i). [a]. Mafao ya Uongozi. (1Thes. 5:12,13, Ebr. 13:17, 1Pet. 5:2-4, 1Kor. 9:10)
- Heshima katika jamii. (Social status)
- Kutambuliwa na kueleweka (recognition and position)
- Mapato. (Material gain)
- Mamlaka (Power and authourity)
- Kuwa na mvuto kwa watu (Influence on large scale)
- Mafao ya kiroho. (Spiritual benefits)

[b]. Kutawala vema mafao ya uongozi.
- Uuone uongozi kama dhamana.
- Uwe na nia ya utumishi.
- Jifunze kutofautisha kati ya mambo yako binafsi na cheo. Panga maisha ambayo unaweza kuishi bila cheo.
- Wekeza kwa ajili ya siku za mbele.
- Uwe tayari kumpisha mwingine kuchukua cheo chako, andaa viongozi.
- Mwamini Mungu katika nafasi uliyo nayo.

ii). [A]. Gharama ya Uongozi.
- Kujitoa muhanga kwa ajili ya wengine. (personal sacrifice)
- Mateso ya kibinafsi – kutokana na hisia mbalimbali.
- Kukataliwa, kukatishwa tamaa, kuchekwa na kuzomewa nk.
- Kulaumiwa
- Kudhalilishwa
- Matatizo ya ndoa na familia
- Kuingiliwa katika maisha kwa mambo binafsi
- Upweke
- Kuwa tayari kushindwa
- Kuwa tayari dhidi ya majaribu yanayotokana na fedha, zinaa na matumizi mabaya ya madaraka nk.

[B]. Kukabiliana na gharama za madaraka/uongozi.

Mjue sana Mungu na kumpenda. (Fil. 3:8-10)
- Jiandae kukabiliana na gharama hizo. (Fil. 1:27-29)
- Tumia muda wako vizuri kwa mambo yote, yaani uwe na kiasi. (Kol. 4:5, Ef. 5:15,16)
- Uwe tayari kuwajibika.
- Uwe mtu wa maombi, ili kumshirikisha Mungu mambo yote na kumtegemea. (Zab. 37:2-7,23)

iii). [a]. Anasa au Majaribu ya uongozi. (vikwazo)

Uongozi huambatana na anasa zake, ambayo ni mitego na majaribu kwa kiongozi.
Baadhi ya majaribu ni:-
- Kujiona umefika juu ya kilele (kiburi). (Isa. 14:13,14. Mithali 29:23)
- Kushindwa kuendelea kuwa na maono. (Mithali 29:18)
- Kuacha kuwa mfano wa kuigwa.
- Kutumia madaraka kwa faida binafsi.
- Kukataa kujipima mwenyewe.
- Kuridhika na utendaji usioridhisha.
- Kutumia vibaya madaraka kwa watu.
- Zinaa.
- Kujisifu na kujiinua.
- Wivu.
- Kutojali familia.
- Uvivu, kukosa motisha na kuahirisha mambo.
- Kujisikia huwezi na hufai.
- Kupoteza dira ya uzima wa milele.

[b]. Kukabiliana na anasa, mitego na majaribu ya uongozi.
(2Tim. 4:15,16, 1Thes. 4:1, 1Thes. 5:17,18, Fil. 4:6,7)

- Kukaa katika maadili mema ya kikristo
- Kudumu na kutii Neno la Mungu
- Maombi. (Mith. 16:3) “Mkabidhi Bwana kazi zako, na mawazo yako yatathibitika”.
- Kuhusisha mambo yako kwa walio karibu nawe, watu au timu yako ya uongozi kwa ushauri. (Mith. 20:18) “Kila kusudi huthibitika kwa kushauriana; Na kwa shauri la akili fanya vita” (Mith. 15:22)








SEHEMU IV



7. SIRI YA MAFANIKIO YA UONGOZI WA KIROHO

Pamoja na kuwa na maadili bora, mambo yafuatayo ni muhimu sana kwa kiongozi.
i. Kumwamini na kumpenda Mungu. (Yoh. 14:1, 12,21,23)
ii. Kufanya mapenzi ya ya Mungu. (Mat. 7:21, Ef. 5:10)
iii. Maombi. (Lk. 18:1, 1Tim. 2:1, Lk. 6:12, Mk. 1:35-39, Ebr. 5:7-10, Ezr. 8:21-23)
iv. Kuwa na Mipango mizuri. (Lk. 14:28-32, 1Tim. 3:15)
v. Kujali rasilimali ulizonazo, pamoja na muda. Kut. 10:25-26,8,9, Lk. 22:35,36, Ef. 5:15,16)
vi. Mahusiano bora na wengine wanaokuzunguka. (Ebr. 12:14,15, Yoh. 13:34,35)

8. MAONO NA MALENGO YA KIONGOZI

Malengo ni tofauti na Maono.

A]. Maono ni uwezo wa kupata picha ya mambo ya siku za mbele.

Ni kufanya safari toka kwa unayoyaona sasa kwa yasiofahamika na kuyaona kama yapo.

Mfano tunajifunza ya kuwa:-
- Nuhu aliona mapema gharika juu ya uso wa nchi akawaonya watu wake. (Mw. 6:13-17,22)
- Yusufu aliona miaka saba ya njaa kabla ya kutokea. (Mw. 41:28-30)
- Musa aliona nchi ya ahadi. (Kut. 3:3-9)
- Nehemia aliona Yerusalemu mpya. (Neh. 1:2-6, 2:3-5)
- Paulo aliona Makedonia inahitaji injili. (Mdo. 16:9,10)
- Nawe unaona maono gani? Juu ya kanisa na familia yako, na mengine?

B]. Baada ya kuona maono.

Ni lazima mambo yafuatayo yafanyike ili maono yawe mambo au kitu halisi na wala si ndoto za kupita tu.
- Kufanyika kazi ya kuhamasisha. Utahitaji mtu au watu katika kuyatimiza mambo uliyoyaona. Musa alihitaji kuwaona wazee wa Israeli kwanza. (Mw. 3:16-18, 4:29,31) Hivyo ivyo, Nehemia, katika sura 2:17-18 katika kitabu cha Nehemia.
- Kuweka malengo, mipango ya utekelezaji ili kuyafikia hayo maono. Pasipo malengo, na mipango mizuri watu watashindwa kuyafikia maono, na hawawezi kuhamisika kuendelea mbele kuyatekeleza. Hatimaye kila mtu atafanya anavyoona machoni pake mwenyewe. (Amu. 21:25)

C]. Msingi wa Biblia kuhusu kuweka malengo.

Yesu alitoa mfano wa mjenzi wa mnara na mfalme aendaye vitani. (Lk. 14:28-32)
Mjenzi katika kuweka malengo, inamlazimu, kuchora ramani, kukusanya vifaa, na rasilimali zingine, kisha kuanza kujenga hatua kwa hatua.
Mpiganaji, kabla ya vita hujiandaa, huandaa majeshi, vifaa, silaha na njia za kuendelea na hivyo hujipanga kikamilifu kabla yayote kwa nia ya kupigana.
Mpango wa Mungu wa wokovu ulikuwa na malengo na mipango yake ya utekelezaji.
- Mungu aliandaa Mtu mmoja, ambaye ni Ibrahimu, baba wa imani
- Taifa la Israel kuwepo
- Manabii
- Yesu kuzaliwa awe mwokozi wa ulimwengu
- Mitume
- Roho mtakatifu
- Kanisa. Hatimaye Wokovu wa milele (Uzima wa milele).

D]. Faida ya kuweka malengo na mipango.

i). Huwezesha kuwa na mwelekeo wa mambo/kazi katika maisha.

Watu wasio na malengo hawafiki popote. Malengo na mipango hufanya maisha yawe ya maana na huweka mwongozo wa maisha.
Kama hujui unakokwenda, njia yoyote itakufikisha huko usikokujua”.
Ukilenga hewa utafanikiwa kupiga shabaha hiyo, na hakuna anayelenga hewa akaikosa”.

ii). Huhamasisha mambo kufanyika.

Viongozi wengi waliofaulu wanakiri kuwa walihamasika na malengo waliyokuwa nayo, na kujiona wakitembea kuelekea katika malengo hayo. Ni malengo yanayowaelekeza ni wapi wawekeze na kutoa vipao mbele katika mali na rasilimali walizonazo na pia nguvu zao.

iii). Humfanya mtu kuwa na tabia ya kutaka kuona matokeo.

Malengo na mipango humfanya kiongozi awe na hamu ya kuona matokeo yake ya kazi anayoifanya na maendeleo yake yalivyo. Yanamfanya mtu kuweka mkazo katika matokeo, badala ya shughuli zinazofanyika. Kwa sababu hiyo pia husaidia:-
- Kupima utendaji na shughuli za kazi
- Kujua umekwenda umbali gani?
- Kuwajibika
- Kutadhimini kazi mara kwa mara na kuboresha utendaji.

Hivyo viongozi waliofaulu ni watu ambao wana malengo kwa siku za mbele. Si watu wa kushughulikia matukio tu, au watu wa mambo yaliopita. Huwa hawasubiri mambo yatokee na ndipo wafanye kitu. Ni watu wanaojitahidi kutimiza mambo kwa vile:-
- Wana maono yaliyo wazi.
- Hujiwekea mipango na ratiba ya kutimiza maono hayo.
- Wanawajibika katika kufuatilia malengo yaliyowekwa.
- Huvumilia wakati maono, malengo, na mipango. Hukutana na vikwazo mbalimbali, na kutotimizwa waliyoyakusudia kwa wakati uliokusudiwa.
- Hutafuta ufumbuzi na kubuni njia ya kuendelea mbele si kurudi nyuma na kukata tamaa.

Kuna viongozi wa aina mbili. Wale wanaosababisha mambo kutokea, na wale wanaosubiri mambo yatokee.

i. Viongozi wanaosababisha mambo yatokee
wana mtazamo wa mbele
wako tayari kupanga mipango, kuona jinsi gani watayatimiza hayo maono yaliyopo.
Wanaweka mikakati ya kuzuia matatizo yatakayoweza kutokea.

ii. Viongozi wanaosubiri mambo yatokee.
hawafanyi chochote , bali wanasubiri mambo yatokee, ndipo wajishughulishe
hutumia muda mwingi kushughulikia matukio.
Ni wazima moto na kutumia muda mwingi kuzima moto kiasi cha kufanya hata wasiweze kujiuliza kwa nini moto unatokea?

Tofauti kubwa kati ya viongozi wa aina hii ni uwezo katika kuweka malengo na kujishughulisha na mipango pia mikakati mbalimbali katika kutimiza maono yaliopo.

Maono, malengo na mipango lazima yawe SMART. Yaani sifa zenye:-
-- Spirit led and Specific - Uongozi wa Roho na yenye shabaha.
-- Measurable - kunapimika
-- Attainable - kufikika
-- Realistic - halisi
-- Time targeted - muda maalum.

Maono yanaweza kushindikana kufiwa kutokana na kuwa, hayakuwa na shabaha maalum, wala hayapimiki, tena sio rahisi kufikika na huenda sio halisi kibinadamu. Labda hayakutengewa muda maalum, yangekuwa na muda yangeweza kuhimizwa na kukamilishwa haraka na hivyo kufurahia matokeo yake. Mawazo (maono) yako yafafanuliwe kwa maneno yako, maneno yazae matendo na tabia (malengo, mipango na mikakati). Hatimaye yataoneka Matokeo kamili (kitu halisi) kutokana na mawazo uliokuwa nayo. Bila kujitahidi kufanya hivyo, mawazo au maono yako yatakuwa sawa na ndoto za mchana, yasiyoweza kufikiwa au kutekelezeka kamwe na mtu yeyote.

Hivyo basi kiongozi wa kiroho huwa na mtazamo wa kimungu. Kama vile Mungu Mwenyenzi alivyo na maono thabiti tangu mwanzo hadi mwisho wa kazi zake katika ulimwengu huu na ujao. Mipango yake katika mikakati ya wokovu imekuwa na ushirikishwaji wa mwanadamu na kwa uwazi kabisa.

Rumi. 8:28: ”Nasi tunajua ya kuwa katika mabo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake”. Yeye ni Mungu anayeenda kwa muda na majira alioyakusudia tangu Adamu kuumbwa hadi Yesu Kristo na hata mwisho wa dunia na hukumu ya ulimwengu. Kazi na matukio tunayoyaona ni yale yaliyotabiriwa na manabii tangu hapo awali. Kwa hiyo Uongozi wa kiroho unabeba sura ya Mungu mwenyewe kwa wana wa Mungu wanaomtegemea.

Biblia inasema hivi:
- Mith. 16:4: “Mkabidhi Bwana kazi zako na mawazo yako yatathibitika.”
- Rumi. 8:14: “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu.”
- Yoh. 15:6: “Akaaye ndani yangu (Yesu) nami ndani yake huyo huzaa sana; pasipo mimi (Yesu) ninyi hamuwezi kufanya neno lolote.”
- Isaya 14:24: “Bwana wa majeshi ameapa, akisema, Hakika yangu kama vile nilivyoazimia, ndivyo itakavyokuwa, na kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyotokea.
- Math. 28:20: “…Tazama, nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari.”


Amina